To unleash the progressive power of a generation of Africans to reach beyond themselves and change the face of the continent forever. This is our time!

  • This is africamotivation.blogspot.com

    Watu wengi sana wamepotezwa mwelekeo wa maisha yao kwa sababu ya kushindwa kabisa kusema hapana kila inapobidi.Hiin ndio maana watu wengi sana wamepoteza muda wao kwa mambo ambayo hayachangii kabisa katika maisha yao na katika malengo yao by mr motivation - africamotivation.blogspot.com

  • This is africamotivation.blogspot.com

    Ni lazima uwe mtu ambaye una ujasiri wa kukataa mambo amabyo hayana msaaada katika malengo yako makubwa by mr motivation - africamotivation.blogspot.com

  • This is africamotivation.blogspot.com

    Muda waklo wa kuishi duniani ukipotea basi ujue hauwezi kabisa kuurudisha tena,hivyo ni lazima uamue kuutumia kufanya mambo ya msingi tu mr motivation by - africamotivation.blogspot.com

  • This is africamotivation.blogspot.com

    uwe mtu mwenye ujasiri wa kusema HAPANA kwa kila kitu ambacho unaona kinakuondolea mweleko uliioukusudia katika maisha yako by mr motivation - africamotivation.blogspot.com

  • This is africamotivation.blogspot.com

    Dont be shy and sad to let them go, if they are nothing to you dont hesitate by mr motivation - africamotivation.blogspot.com

Hance Mligo

Share:
To unleash the progressive power of a generation of Africans to reach beyond themselves and change the face of the continent forever. This is our time!
Share:

Audio>>pupa vs njia panda

Share:

Audio>>safari mafanikio

Share:

Audio>>Utafiti

Share:

» MJUE KIJANA ALIYEANZA KUMILIKI KAMPUNI AKIWA NA MIAKA 16,msome hapa kumjua na ujifunze mengi zaidi.

Kuna kijana anaitwa odense miaka 22
kutoka nchini Uganda anaeitwa Andrew
Mapuya.
Andrew anatokea katika famili ya chini sana
ambapo mwaka 2008 wazazi wake woote
walisimamishwa kazi.Jambo ambalo
lilipelekea nyumbani maisha kuwa
magumu.Wakati huo akiwa na miaka 16 na ni
mwanafunzi wa sekondari ikawa inamlazimu
aokote chupa za plastic auze na anunue
chakula cha nyumbani kwao.
Mwaka huo huo serikali ya Uganda ilipiga
marufuku matumizi ya mifuko ya plastic kwa
sababu za kimazingira pamoja na kiafya.Bila
kupoteza muda Andrew akatambua fursa kuwa
iwapo hakutauzwa mifuko ya plastic bado
mifuko itahitajika je mbadala wake ni nini?
Akawaza aanzishe biashara ya kutengeneza
mifuko ya karatasi yaani paper bag.Akafanya
ufatiti wa uhitaji wake wa mtaji ikawa ni tsh
za
uganda 36,000.Basi akaanza mdogo mdogo
kukusanya chupa za plastic anauza hela
anatunza ili kupata mtaji.Akatunza pesa
mpaka
alipobakiwa na kiasi kidogo kama tsh 11,000
akaenda kumuomba mwalimu shule
akampatia.Mwaka huo huo akasajili kampuni
yake ambayo inasemekana ndio kampuni ya
kwanza kusajiliwa ya kutengeneza na kuuza
mifuko ya karatasi.Kampuni inaitwa Youth
Enterprenual Link Investment (YELI)
Kampuni hiyo sasa inawateja wengi na
inatengeneza na kusambaza mifuko kwenye
super markets,restaurant,medical
centre,maduka,na makampuni mbali mbali
katika mji wa Kampala.Mpaka sasa
ameshaajiri
vijana zaidi ya 16.
Mwaka 2012 alikuwa mshindi wa shindano la
Anzisha Prize la vijana wajasiriamali na
alishinda dola za kimarekani 30,000
Ninachoweza kuona kama funzo kutoka kwa
kijana huyu ni kuwa
1.Unapotaka kuanzisha biashara fanya utafiti
2.Fanya biashara kwa kuangalia uhitaji wa
bidhaa husika yaani jamii inapungukiwa kitu
hicho
3.Kunapokuwa na shida ya kitu flani sehemu
flani hiyo ni Fursa ina maana unatakiwa
kuanzisha baiashara ili utoe suluhisho,ili utoe
huduma na automatical ndio biashara sasa
maana ina wateja.
4.Kwa vijana usisubiri mpaka uwe mtu mzima
ndio uanzishe biashara.Anzakuwaza mafanikio
sasa,anza kupanua mawazo yako na uchukue
hatua
Asante kwa kutembelea blog yako ya africa motivation
*@mr motivation*
Share:

JE, NINI CHA KUFANYA USIPOONA MATUNDA YA KAZI UIFANYAYO

Unakumbuka wakati unaanza kazi, kuna vitu
ambavyo ulitamani sana kuwa navyo,
ulitamani kuwa na chumba chako, angalau
chumba na sebule, kitanda, TV, kajiko ka gesi,
na vikorokocho vya ndani. Hembu angalia vile
vitu kama unavyo au huna na ulivipataje,
jiulize baada ya kuvipata pesa ya mshahara
uliyotumia kununua vile vitu iko wapi kama
sasa hivi huvinunui tena? Unajua ni kwanini
ulivipata hivyo vitu?
Huna haja ya kuumiza kichwa sana, ulivipata
kwakuwa ulikuwa na malengo na mtu
anapokuwa na mlengo flani basi moja kwa
moja huilazimisha akili yake kufanyakazi
kuelekea yale malengo. Kuna namna mbili za
kuweka malengo, namna ya kwanza ni kuweka
malengo bila kujijua “Unconscious Goals” aina
ya pili ni kuweka malengo ukiwa unajijua
“Conscious Goals”.
Aina hii ya kwanza ni ile ambayo kuna vitu
unapanga kuvifanya lakini si kwa mpangilio
au hukai chini ukasema haya ni malengo
yangu. Kama ambavyo ulisema unatamani
kununu TV na ukanunua hayo ni malengo
ambayo ulijiwekea, aina ya pili ni ile ambayo
unakaa chini na kuandika au kusema kabisa
mwaka huu nataka kufanya kitu A, B, Cna D.
Katika maisha mafanikio au vitu havidondoki
tu kama mvua ni lazima uviwaze na
kuviwekea malengo iwe ni kwa kujua kuwa
haya ni malengo au si malengo. Kwa watu
wengi ambao hawafanikiwa wanajikuta kuwa
badala ya kuweka malengo basi huweka
vikwazo. Kwamba kwa kuangalia mshahara
wako badala na kuuona mdogo badala ya
kuweka melango kutokana na mshahara wako
mdogo basi unajiweka vikwazo kutokana na
mshahara wako mdogo.
Hembu nifafanue kidogo, tuchukulia unapata
mshahara wa shilingi laki mbili kwa mwezi na
akiba ni shilingi elfu hamsini, kwa maana
kuwa hata ukijibana vipi utabakia na shilingi
elfu hamsini. Sasa umepata kiwanja cha
shilingi milioni moja, watu ambao
hawafanikiwi watawaza hivi “Mshahara wangu
mdogo siwezi kununua kiwanja cha milioni
moja”.
Lakini watu waliofanikiwa huweza hivi “Milioni
moja nikikusanya elfu hamsini hamsini, kwa
mwaka nitakuwa nalaki sita, hizi laki nne
zilizobaki kununua kiwanja ...ngoja niangalie
ofisini…siwezi pata mtu wa kunikopesha
kweli…hapa nikipunguza kupanda Bajaji…vipi
nikiwa napika mwenyewe si nita save…na
nikiuza na ile deki ya CD ambayo siitumiii…si
zitafika kweli…kuna na lile dili ofisini ngoja
ni….”
Umeona tofauti ya watu hawa wawili, yule
wakwanza baada tu ya kuona kuwa elfu
hamsini haitoshi kununua kiwanja cha milioni
moja alikaa kimya akasahau na
kujisahaulisha tena kuhusu kiwanja. Tena
utamsikia akisema “Sitaki kujipa tamaa za
bure, haya maisha ni lazima uridhike na
unachopata…” Lakini wapili yeye ataumiza
kichwa mpaka kupata anachokitaka, hivyo
ndivyo unavyotakiwa usiangalie usicho nacho
bali namna ya kupata cha kuongezea.
Asante kwa kutembelea blog yako ya makinspire.blogspot.com. karibu tena kwa kujifunza mengi zaidi
*@Mr motivation*
Share:

Video>>One of The Most Inspiring Speeches

Share:

Video>>THE WINNING MENTALITY - Powerful Motivation 2017

Share:

GET LATEST MOTIVATION AND INSPIRATION UPDATES VIA EMAIL

Enter your name and e mail.

Popular africa motivation posts

Recent africa motivation posts