-
This is africamotivation.blogspot.com
Watu wengi sana wamepotezwa mwelekeo wa maisha yao kwa sababu ya kushindwa kabisa kusema hapana kila inapobidi.Hiin ndio maana watu wengi sana wamepoteza muda wao kwa mambo ambayo hayachangii kabisa katika maisha yao na katika malengo yao by mr motivation - africamotivation.blogspot.com
-
This is africamotivation.blogspot.com
Ni lazima uwe mtu ambaye una ujasiri wa kukataa mambo amabyo hayana msaaada katika malengo yako makubwa by mr motivation - africamotivation.blogspot.com
-
This is africamotivation.blogspot.com
Muda waklo wa kuishi duniani ukipotea basi ujue hauwezi kabisa kuurudisha tena,hivyo ni lazima uamue kuutumia kufanya mambo ya msingi tu mr motivation by - africamotivation.blogspot.com
-
This is africamotivation.blogspot.com
uwe mtu mwenye ujasiri wa kusema HAPANA kwa kila kitu ambacho unaona kinakuondolea mweleko uliioukusudia katika maisha yako by mr motivation - africamotivation.blogspot.com
-
This is africamotivation.blogspot.com
Dont be shy and sad to let them go, if they are nothing to you dont hesitate by mr motivation - africamotivation.blogspot.com
» MJUE KIJANA ALIYEANZA KUMILIKI KAMPUNI AKIWA NA MIAKA 16,msome hapa kumjua na ujifunze mengi zaidi.
JE, NINI CHA KUFANYA USIPOONA MATUNDA YA KAZI UIFANYAYO
» UJASILI,KUJIAMINI-PANDA MBEGU YA UJASIRI KWA WALIO CHINI YAKO, soma hapa ujifunze jinsi unavyoweza kupandikiza mbegu ya ujasili.
» MAMBO MAZURI MUDA MWINGINE HUPITISHWA KWENYE NJIA MBAYA,soma hapa kujifunza mengi na update hamasa

Hivi umewahi kumuona mdudu kiwavi, kiwavi
ni mdudu mwenye sura mbaya sana na
mwenye umbo baya sana, kwasababu
anapokuwa kwenye harakati za ukuaji
anakuwa kama mfano wa jongoo, lakini kitu
kimoja ambacho kinanishangaza kutoka
kwenye huyu mdudu ni kwamba ni yeye huyu
huyu ambae siku moja anakuja kuwa kipepeo,
najiuliza tu swali moja unadhani kwa kipindi
hajawa kipepeo angesema basi bora nife kama
ndo niko hivi,kipepeo angetokea?laa hasha
asingetokea, angesema mimi ndo nimeumbwa
hivi hivi na maisha yangu ndo haya haya
Mungu kanionea namatumaini leo
tusingeuona uzuri wa kipepeo.
Na maisha yetu ndivyo nalivyo muda
mwingine mambo mazuri huwa yanapita
kwenye matukio mabaya ambayo huenda
huyapendi, siku moja alikuepo jamaa mmoja
alikuwa amechoka kabisa kufanya kazi
ambayo anaifanya, huenda ni kama wewe
ulivyochoka kwenda kazini kwasababu
unaamka mapema sana, huyu bwana kila siku
akawa anamuomba Mungu apate kazi kubwa ,
nzuri na yenye mshahra zaidi ya ule ambao
alio nao kwasasa.lakini apate kazi
ambayoatakuwa na furaha, aliomba saana tu,
siku moja Mungu akajibu dua yake, alipewa
kazi na boss akachelewa kuiwasilisha
kampuni ikakosa tenda, basi kesho yake
alipofika kazini alikuta barua ya kufukuzwa
kazi.
Daaah jamaa alilia sana sana tu kwanini
amefukuzwa kazi, familia yake itaishije,
siunajua wafanyakazi huwa wakiwa kazini
wanakuwa wameridhika eee hawawazi hata
kufanyabiashara au mambo yanaweza
kuwaingizia kipato cha ziada kwa muda wa
ziada, basi alilia sana nakuanza kumlalamikia
Mungu kuwa amemuomba apate kazi sasa
ndo kafukuzwa kabisa.
Baada ya kuteseka kwa muda kidogo na
maisha kuwa magumu kwaajili ya kufukuzwa
kazi akapata muda wa kuwa anasoma
magazeti kupoteza mawazo, siku moja
akakuta gazeti kuna kampuni imeanzishwa
anatakiwa mfanyakazi mwenye sifa kama
zake, akaenda kufanya usaili akafanikiwa
kupata kazi, akapata cheo kama kile kile
alichoomba kwa Mungu, mshahara ule ule na
akawa free, sasa tujifunze kitu unadhani
aisingefukuzwa kazi angepata muda wa kukaa
kusoma gazeti na kupata habari iyo kiukweli
ingekuwa ngumu.
Rafiki usihuzunike unapokuwa kwenye wakati
mgumu, kwenye wakati ambao Mambo
hayaendi sawa, jua Mungu anakutafutia nafasi
iliyobora zaidi endelea kupambana hadi
kileweke, dhahabu ili ing'ae sharti ichomwe
moto, usikate tamaa usihuzunike siku moja
utakuja kuishi maisha yaliyo bora.
USIHUZUNIKE MDUDU KIWAVI, SIKU MOJA
UTAKUWA KIPEPEO
*@Mr motivation*
WATANZANIA NA TABIA YA KULALAMIKA NA KULAUMU, soma hapa kujifunza mengi na kuacha tabia ya kulaumu na kulalamika
ukosefu wa mitaji ya kuendesha biashara.
Watu wanalalamika eti hawafikiriwi, hakuna anayewajali na hawasaidiwi! Yawezekana ni kweli, lakini kwa yeyote mwenye malalamiko na aketi chini na ajiulize hili; “Ndiyo hakuna anayenijali, hakuna anayenifikiria na hakuna anayenisaidia, kwahiyo…...”
Ukishajiuliza swali la “kwahiyo…” --bilashaka utaamua mojawapo kati ya haya:
ama ni kuacha kufanya biashara au kuendelea na biashara”. Endapo utaamua kuacha biashara kero na malalamiko yako yote vitakuwa vimeishia hapo na kimsingi utaweza kuendelea na maisha mengine.
Endapo utachagua kuendelea na biashara, maana yake ni kwamba matatizo unayolalamikia si makubwa kiasi cha kukuzuia kupata faida na pengine ndiyo maana umechagua kuendelea na biashara bila kujali matatizo na changamoto zilizopo.
Utamaduni wa kulalamika juu ya kazi tunazozifanya tumeurithi kutoka kwa watumishi hasa waajiriwa. Mfumo wa ajira duniani uko katika umbo la pembe tatu (piramidi). Ambapo unakuta mkubwa ni mmoja na chini yake kunakuwa na watu wengi kutegemea na ukubwa wa taasisi au kampuni husika iliyokuajiri. Mara nyingi watu walioko chini wakishindwa jambo lolote umsukumia yule aliyejuu ili afikiri na kutoa suruhisho kwaniaba ya wale wote anaowaongoza.
Kwa maana nyingine ni kwamba katika umbo hilo hapa juu, kuna mambo mengine huruhusiwi kuyafanya au kuyatolea maamuzi isipokuwa aliye juu yako. Pili, ukiwa mwajiriwa wa ngazi za chini kuna mambo ambayo yakikushinda unayapeleka kwa mkubwa wako kwaajili ya ufumbuzi zaidi.
Kwahiyo, chimbuko la tabia ya kulalamika ni utaratibu wa kutegemea maamuzi ya aliye juu yako. Kama anayepaswa kuamua jambo fulani, hafanyi hivyo kwa wakati au akafanya maamuzi vibaya basi utakuta waajiriwa walioko chini wanafanyakazi kwa kunung’unika muda wote, wanalalamika muda wote wanasema hovyo muda wote na hasa wakiwa maeneo ya nje ya ofisi zao.
Ikumbukwe kuwa, kinachowapa waajiriwa uhalali wa kulalamika ni ule mfumo au utaratibu wa ajira duniani ambao unatoa nafasi kwa mwajiriwa kuweza kupeleka malalamiko yake ngazi za juu endapo ataona kuna mambo ambayo hayaendi sawa.
Katika mfumo mzima wa ajira “MKUU” ni mtu wa mwisho na hatutarajii halalamike kwasababu hakuna mtu mwingine aliye juu yake ambaye anatakiwa kumpelekea malalamiko, ingawaje wengine ujikuta nao wakilalamika kwa watu wa chini yao. Wewe kama ni “Mkuu” kazi yako ni kuamua na kutenda basi!
*@Mr motivation*