Mbona unalalamika kila siku kwamba biashara yako ni ngumu? Kwani wewe
ulianzisha biashara yako kwa lengo gani? Malalamiko kutoka kwa
wajasiriamali imekuwa ni sehemu ya Maisha yao. Kila unapojaribu kuongea
na wajasiriamali lazima usikie malalamiko mengi ikiwemo--
ukosefu wa mitaji ya kuendesha biashara.
Watu wanalalamika eti hawafikiriwi, hakuna anayewajali na hawasaidiwi!
Yawezekana ni kweli, lakini kwa yeyote mwenye malalamiko na aketi chini
na ajiulize hili; “Ndiyo hakuna anayenijali, hakuna anayenifikiria na
hakuna anayenisaidia, kwahiyo…...”
Ukishajiuliza swali la “kwahiyo…” --bilashaka utaamua mojawapo kati ya haya:
ama ni kuacha kufanya biashara au kuendelea na biashara”. Endapo utaamua
kuacha biashara kero na malalamiko yako yote vitakuwa vimeishia hapo na
kimsingi utaweza kuendelea na maisha mengine.
Endapo utachagua kuendelea na biashara, maana yake ni kwamba matatizo
unayolalamikia si makubwa kiasi cha kukuzuia kupata faida na pengine
ndiyo maana umechagua kuendelea na biashara bila kujali matatizo na
changamoto zilizopo.
Utamaduni wa kulalamika juu ya kazi tunazozifanya tumeurithi kutoka kwa
watumishi hasa waajiriwa. Mfumo wa ajira duniani uko katika umbo la
pembe tatu (piramidi). Ambapo unakuta mkubwa ni mmoja na chini yake
kunakuwa na watu wengi kutegemea na ukubwa wa taasisi au kampuni husika
iliyokuajiri. Mara nyingi watu walioko chini wakishindwa jambo lolote
umsukumia yule aliyejuu ili afikiri na kutoa suruhisho kwaniaba ya wale
wote anaowaongoza.
Kwa maana nyingine ni kwamba katika umbo hilo hapa juu, kuna mambo
mengine huruhusiwi kuyafanya au kuyatolea maamuzi isipokuwa aliye juu
yako. Pili, ukiwa mwajiriwa wa ngazi za chini kuna mambo ambayo
yakikushinda unayapeleka kwa mkubwa wako kwaajili ya ufumbuzi zaidi.
Kwahiyo, chimbuko la tabia ya kulalamika ni utaratibu wa kutegemea
maamuzi ya aliye juu yako. Kama anayepaswa kuamua jambo fulani, hafanyi
hivyo kwa wakati au akafanya maamuzi vibaya basi utakuta waajiriwa
walioko chini wanafanyakazi kwa kunung’unika muda wote, wanalalamika
muda wote wanasema hovyo muda wote na hasa wakiwa maeneo ya nje ya ofisi
zao.
Ikumbukwe kuwa, kinachowapa waajiriwa uhalali wa kulalamika ni ule mfumo
au utaratibu wa ajira duniani ambao unatoa nafasi kwa mwajiriwa kuweza
kupeleka malalamiko yake ngazi za juu endapo ataona kuna mambo ambayo
hayaendi sawa.
Katika mfumo mzima wa ajira “MKUU” ni mtu wa mwisho na hatutarajii
halalamike kwasababu hakuna mtu mwingine aliye juu yake ambaye anatakiwa
kumpelekea malalamiko, ingawaje wengine ujikuta nao wakilalamika kwa
watu wa chini yao. Wewe kama ni “Mkuu” kazi yako ni kuamua na kutenda
basi!
*@Mr motivation*
Home »
motivation and inspiration
» WATANZANIA NA TABIA YA KULALAMIKA NA KULAUMU, soma hapa kujifunza mengi na kuacha tabia ya kulaumu na kulalamika
No comments:
Post a Comment